MHANDISI MANALA T MBUMBA ASHIRIKI ZOEZI LA KUHITIMISHA KAMPENI ZA CCM KAGONGWA | NEWS PLANET

Wednesday, November 27, 2024

MHANDISI MANALA T MBUMBA ASHIRIKI ZOEZI LA KUHITIMISHA KAMPENI ZA CCM KAGONGWA

  Sammy Media       Wednesday, November 27, 2024




Na SAMUEL SAMSONI



Mwenyekiti wa Taasisi ya Manala Foundation na mdau wa Maendeleo manispaa ya kahama, Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Manala T. Mbumba ameshiriki zoezi la kuhitimisha kampeni za CCM katika Kata ya Kagongwa huku akitembelea vitongoji mbalimbali kikiwemo kitongoji cha Kishima, na Kagongwa akiwa na lengo la kuongeza hamasa katika kampeni hizo

Wakati wa zoezi hilo Mhandisi Manala amekutana na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga akiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga CDE Benard Werema, Katibu wa hamasa Mkoa wa Shinyanga CDE Anord Bweichum, pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba.

Licha ya kufika katika Kampeni hizo Mhandisi Manara ameungana na viongozi hao kuwaombea wagombea wao kura katika uchaguzi unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024

Zoezi lilitamatishwa vyema baada ya hotuba ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga CDE Benard Werema ikiwataka viongozi watakaochaguliwa kuwatumikia wananchi kwa kutatua changamoto zao

"... Ninajua tayari mmeshashinda uchaguzi, hivyo keshokutwa tuu mtaanza kuletewa kero ofsini, Nendeni mkawatumikie wananchi" Amesema Werema
Baadhi ya picha za Mwenyekiti wa Taasisi ya Manala Foundation Mhandisi Manala T. Mbuba katika matukio mbalimbali wakati wa kuhitimisha kampeni za CCM Kagongwa





















logoblog
Previous
« Prev Post