TAKUKURU KAHAMA WATANGAZA MOTO KWA WATAKAOHUSIKA KATIKA VITENDO VYA RUSHWA UCHAGUZI | NEWS PLANET

Monday, November 11, 2024

TAKUKURU KAHAMA WATANGAZA MOTO KWA WATAKAOHUSIKA KATIKA VITENDO VYA RUSHWA UCHAGUZI

  Sammy Media       Monday, November 11, 2024


Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilayani Kahama mkoani Shinyanga Abdalah Urari


TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Kahama mkoani Shinyanga imewaonya wagombea pamoja na wananchi watakaojihusisha na vitendo vya Rushwa katika kipindi chote cha uchaguzi, ukitangulia uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024 na serikali kuu 2025


Ofisa wa Takukuru kutoka wilayani hapo ambaye ni mchunguzi wa Masuala ya rushwa Mlamuzi Pius Kuhanda ameyasema hayo leo tarehe 11,Novemba,2024 alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu mwelekeo wa uchaguzi wa serikali za mitaa Kuhanda amesema rushwa ni kosa la maadili na ni kosa la kiimani ambalo linapaswa ukemewa kwa nguvu zote. 

Kuhanda ameongeza kuwa baadhi ya viongozi wanaotoa ushawishi kwa njia ya pesa,vitenge, Sabuni au tisheti huku akitaja baadhi ya viashiria vya rushwa kuwa ni pamoja na waliopitishwa kugombea nafasi mbali mbali kujiengua na kutoshiriki katika uchaguzi, kuwepo kwa machawa wengi wanaopewa pesa na baadhi ya wagombea kisha kuzisambaza kwa baadhi ya wapiga Kura pamoja na wale wananchi wanaodai unatuachaje.


Kuhanda amesema Uchaguzi huu ni muhimu kwani ni dira inayoonesha muelekeo wa uchaguzi ujao na husaidia upatikanaji wa viongozi bora wanaopelekea kuleta maendeleo katika jamii na kusema kuwa rushwa inamkosesha mwananchi haki ya kikatiba


“Ipo haja ya kuibadilisha jamii kwa mtazamo wa kumuangalia mla rushwa kuwa ni shujaa na mtazamo uwe mla rushwa ni mwenye dhambi” amesema Kuhanda.


Kuhanda alisema kwa mujibu wa Shirika la National Government Social and corrupition Survey na Shirika la Internationa Economic Survey yalifanya uchunguzi mwaka 2020 nakubaini kuwa asilimia 42.7 waliohojiwa walidai wanao anzisha vitendo vya rushwa ni watoa huduma, asilimia 27.2 waliohojiwa walidai wanaoanzisha ni wale wenye uhitaji wa huduma katika taasisi na mashirika mbali mbali huku asilimia 23.5 waliohojiwa walisema watoa huduma na wanaohitaji huduma wote walijihusisha na rushwa.




Mkuu wa TAKUKURU wilayani Kahama Abdallah Urari amesema waandishi wa habari na TAKUKURU wanalojukumu la kuweka mikakati ya pamoja kuzuia rushwa kwa mujibu wa ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza na kusema kuwa licha ya TAKUKURU kupambana na matukio ya namna hiyo wanaanza kwa kutoa elimu katika makundi mbalimbali ambapo mpaka sasa wameshafikia makundi mbali mbali likiwemo kundi la Boda boda, kundi la Viongozi wa dini, mashuleni, pamoja na waandishi wa habari ambao wametajwa kuwa nyenzo muhimu ya kuihabarisha na kuielimisha jamii kupitia vyombo vyao wanavyovitumikia.


“Rushwa ni adui wa Maendeleo, Ibara ya tisa (S) ya katiba hiyo hiyo inaelekeza kwamba mamlaka ya nchi na taasisi zake zinahakikisha juhudi zote. za kutokomeza rushwa nchini” amesema Urari.


Ofisa kutoka Takukuru na Mchunguzi kutoka Wilaya ya Kahama Happnes Bilakwate amesema wananchi wanatakiwa kupitia na kusoma mitandao ya kijamii ya taasisi hiyo ili kujua sheria na vitendo vinavyokatazwa juu ya kupinga vitendo vya rushwa hapa nchini.


"kupitia wadau wetu wa habari mtusaidie kuhamasisha wananchi wafuatilie page ya taasisi kwenye mitandao ya kijamii kama insta,facebook,twiter na uifuate na kubscribe you tube channel ya Takukuru Tv ili kupata habari mbalibali za masuala ya rushwa"amesema Bilakwate.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhia katika mafunzo hayo yaliyotolewa na TAKUKURU Kahama juu ya mwelekeo wa uchaguzi wa serikali za mtaa

Baadhi ya waandishi wa habari na maofisa wa TAKUKURU katika mafunzo hayo yaliyotolewa na TAKUKURU Kahama juu ya mwelekeo wa uchaguzi wa serikali za mitaa

MLAMUZI PIUS KUHANDA (MCHUNGUZI)Wilaya ya KAHAMA akitoa mafunzo yaliyotolewa na TAKUKURU Kahama kwa waandishi wa habari juu ya mwenendo wa uchaguzi wa serikali za mitaa

HAPPY BILAKWATE(MCHUNGUZI) Kahama wakati wa mafunzo yaliyotolewa na TAKUKURU Kahama kuhusu mwenendo wa uchaguzi wa serikali za mitaa

Takukuru inasema kuwa rushwa ni adui wa maendeleo na kwamba kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha inatokomezwa nchini
#Mapambano dhidi ya Rushwa ni jukumu langu na lako timiza wajibu#






logoblog
Previous
« Prev Post